Jumamosi, 10 Februari 2018

UTAWALA WATOA MAELEKEZO YA MWISHO KUHUSU BTP

Na mwandishi
Omben Stony 

Mkuu wa chuo(Principle), Makamu(Vice principle), Muadili mkuu(Dean of students) na Muadili msaidizi(Vice dean of students), katika maandalizi ya BTP wazidi kusisitiza wanachuo wote ambao ni walimu tarajali sasa katika mambo makuu manne ambayo kama wanachuo wayafuate na kuwasaidia kwaajili ya kazi hii ya ualimu kama ifuatavyo;  
                                                                                                                                                            Matumizi mazuri ya fedha ya kujikimu 
Kila mwanachuo lazima awe makini katika matumizi ya pesa yake maana kila maeneo muendako kunachangamoto zake hivyo basi hakikisha bajeti yako inakuwa na mahitaji yenye tija katika mazoezi hayo ya ufundishaji.Lakini pia si vema kutumia vilevi kama pombe na mambo mengine yanayofanana na hilo ili isije kutokea dosari yeyote kwa mtu binafsi na chuo pia kwa ujumla.Tafadhali tumieni pesa zenu katika maadili na hekima nzuri ya fedha, Makamu mkuu wa chuo amezungumza hayo katika neneo la kutaniko (assembly) .

Mahusiano chanya na yenye maana 
Mahusiano katika maisha ni ya muhimu sana lakini ni lazima izingatiwe kwamba hayo mahusiano ni ya mfumo gani na yanatija gani.Hakikisha unakuwa na mahusiano mazuri na wanafunzi wenu ili ili wawe huru kueleza changamoto zao kwako wewe kama mwalimu.Lakini pia mahusiano mazuri kati ya walimu waajiliwa katika shule husika ili kuboresha taaluma ya shule lakini pia huo ndio ubinadamu.Pia chunga sana mahusiano ya kimapenzi ya dharula maana pia yanaweza kukusababishia dosari kwa namna moja ama nyingi, saambamba na hilo napenda kukumbusha kwamba ni marufuku mwalimu na mwanafunzi kuwa na mahusiano ya kimapenzi kama ilivyotamkwa rasmi na waziri wa elimu Mh.Joyce Ndalichako, Alisema muadili mkuu.

Ushirikiano baina ya wanachuo(walimu) na jamii inayo wazunguka
Katika swala zima la mafanikio hasa katika elimu ushirikiano ni wa muhimu sana kwaajili ya maboresho ya elimu.Nendeni huko mkashirikiane katika kila hali ili mtimize kusudi zima la mtaala, pia shirikiana na walimu wazoefu wa pale shuleni ili muweze kujua mengi kuhusu wanafunzi na mazingira kwa ujumla ili tu swala zima la BTP lifanikiwe na kuzalisha MATOKEO MAKUBWA.Pia chukulianeni ninyi kwa ninyi katika mapungufu ya ubinadsmu ili muishi kwa amani bila vikwazo na migogoro baina yenu, tafadhali mkaishi kwa amani.
Kama walimu-wanafunzi nawasihi mkashirikiane kwa kila jambo jema na changamoto, Muadili msaidizi alisema hayo katika kutaniko la wanachuo.

Uwajibikaji
Hakikisha unawajibika ipasavyo katika shule uliyopangiwa na kumbukeni hatuna muda wakupoteza kwa kipindi hiki kwahiyo nenda na uhakikishe unatimiza wajibu wako kwa wakati ili kuepusha dosari za uzembe katika BTP hiyo.Pia hakikisheni mnawasaidia wanafunzi kitaaluma na kiaikolojia mkiwa kama walimu tarajali na uzembe katika kazi hautakiwi, na jaribuni kuendana na mazingira kwa wema.Fanyeni kila jukumu mtakalopewa na wakati na weredi wa kutosha ili chuo chetu kizidi kuwa na sifa nzuri ya kuzalisha walimu bora na si bora walimu.,Alisema mkuu wa chuo.
Nawatakia mazoezi mema ya ufundishaji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

UTAWALA WATOA MAELEKEZO YA MWISHO KUHUSU BTP

Na mwandishi Omben Stony   Mkuu wa chuo(Principle), Makamu(Vice principle), Muadili mkuu(Dean of students) na Muadili msaidizi(Vice d...