Alhamisi, 8 Februari 2018

RAISI SAMWEL O. LALA VIKALI DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

motco newsRaisi wa chuo cha ualimu Morogoro Mh.Samwel O. Lala amewaonya wanachuo vikali kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yaani Facebook,Twiter,Instagram na Whatsap.Kumekuwa na matumizi mabaya ya wanachuo kutumia mitandao ya kijamii vibaya pasipo na hofu yeyote ile bila hata kujali sheria inasemaje katika matumizi ya mitandao.Picha na video zisizofaa katika maadili na rekodi mbali mbali zisizoruhusiwa zimekithiri sana.
Aidha Rais ameonya kuwa ni mwanzo na mwisho kwa mwanachuo kukutwa na kosa hilo la kimtandao au vifaa vya kimtandao na lasivyo sheria itachukua hatua mara moja na kupewa adhabu kali sana.Pia makamu mkuu wa chuo cha ualimu Morogoro ameonya pia katika eneo la kutaniko la wanachuo na kuzungumza kwamba mwanachuo akibainika na makosa hayo basi sheria itafuata mkondo wake na hatokuwa katika mikono ya chuo tena.Makamu huyo alimalizia kwa kusema kuwa angependa kwamba wanachuo wote waishi katika maadili na misingi ya ualimu ili kuifaa jamii ya kitanzania.
                                                                                                                               
                                                                                                                                                                                                                                                                Na mwandishi wetu
                                                                                                                                      Omben Stony

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

UTAWALA WATOA MAELEKEZO YA MWISHO KUHUSU BTP

Na mwandishi Omben Stony   Mkuu wa chuo(Principle), Makamu(Vice principle), Muadili mkuu(Dean of students) na Muadili msaidizi(Vice d...